MGOMBEA WA UMISS AZUIWA KUINGIA UCHINA
Mgombea wa mashindano ya malkia wa dunia kutoka Canada amesema kuwa alizuiwa kupanda ndege ya kuelekea Uchina kutoka Hong Kong.
Anastasia
Lin mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mzaliwa wa Uchina amesema kuwa
hakupata mwaliko kuhudhuria hafla hiyo hatua ambayo ilimzuia kutuma ombi
la kupata viza.Lakini alijaribu kusafiri kuelekea Sanya kupitia Hong Kong,kwa kuwa watalii kutoka Canada hupewa Viza wanapowasili.
Bi Lin amelaumu tukio hilo kwa kampeni zake za kibinaadamu.
Mashindano hayo ya malkia wa dunia yanatarajiwa kufanyika katika hoteli ya kitalii ya Sanya mnamo terehe 19 mwezi Disemba.
Wakati alipotoa malalimishi yake kwamba hakupewa mwaliko,BBC ilijaribu kuwasiliana na mamlaka ya mashindano hayo lakini haikupata jibu lolote.
Category:

0 comments