.

.

JOHN KERRY WAZIRI WA MAMBO YA KIGENI WA MAREKANI N

ZePLAN | 01:48:00 | 0 comments


Urusi
Picha juu John kerry waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani


Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry yumo nchini Moscow kwa mashauriano na Rais Vladimir Putin kuhusu njia za kumaliza vita Syria.

Mazungumzo hayo yanalenga kupunguza ufa kati ya Urusi na Marekani, hasa kuhusu makundi ambayo yanafaa kujuishwa kwenye mazungumzo.

Urusi, ambayo inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad, imesema mkutano wa majuzi wa makundi yanayopinga serikali ya Syria haukuwakilisha makundi yote.

Aidha, Moscow imesema mkutano huo ulijumuisha ‘makundi ya kigaidi’.
Hata hivyo licha ya tofauti kubwa kati ya Urusi na Marekani, Bw Kerry ataweka msingi kwa mazungumzo kati ya mataifa yenye ushawishi duniani kuhusu mzozo huo wa Syria baadaye wiki hii mjini New York.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria yamedumu kwa miaka minne sasa.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments