.

.

UN KUINGILIA KATI SUALA LA WAKIMBIZI SYRIA

ZePLAN | 21:30:00 | 0 comments


 Picha juu wakimbizi wa syria
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa serikali ya Jordan kuwaruhusu idadi ya wakimbizi wanaokadiriwa kufikia elfu kumi na mbili wa Syria ambao wamekwama katika mpaka wake wakiwa wamedhoofika vibaya.

Umoja wa mataifa umesema idadi ya wakimbizi wanaotaka kuingia Jordan imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, ikujumuisha watoto kadhaa,watu wazima na wagonjwa.
Habari kutoka Jordan zinasema kwamba nchi hiyo imefunga njia zote za panya zinazotoa mwanya wa watu kuingia nchini humo kiholela,takriban miezi nane iliyopita na wakimbizi walio wengi wameondoka nchini humo .

Hata hivyo umoja wa mataifa unakadiria kuwa Jordan bado ina idadi ya wakimbizi wapatao laki sita wa Syria.kikundi cha kinachoendesha kampeni cha kutetea haki za binaadamu kimeishutumu Jordan kwa kuhatarisha uhai kwa kuzuia wakimbizi wapya kuingia nchini mwake.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments