Shirika la kutetea haki za Binadamu
Ulimwenguni la Amnesty International,limeituhumu serikali ya Burundi kwa
mauaji watu wasio na hatia na matumizi mabaya ya jeshi la nchi hiyo.
Shirika
hilo limelaani mauaji yaliyotokea Desemba 11 ambapo watu nane waliuawa
wakati jeshi la serikali lilipokuwa likijihami dhidi ya mashambulizi ya
waasi watatu waliovamia vituo vitatu tofauti vya jeshi.
Serikali
ya Burundi iliwaelezea wale waliouawa kuwa ni maadui,jambo ambalo
linapingwa vikali na Amnesty ambao wanasema kuwa wengi wa waliouawa ni
watu wasio na hatia na raia wa taifa hilo.
Ripoti ya shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.
Ripoti ya shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.
Kutokana na hali hiyo Umoja wa Afrika AU unasisitiza
baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha mpango wake wa kupeleka
kikosi cha wanajeshi 5000 wa kulinda amani nchini kufuatia mauaji ya
raia yanayoendelea.
Hata hivyo serikali ya Burundi inapinga hatua hiyo.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments