Shirika la umoja wa Mataifa
linaloshughulikia maswala ya watoto UNICEF, linasema kuwa mashambulizi
kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria na kwenye nchi
zingine yamewalazimu zaidi ya watoto milioni moja kuacha masomo.
Katika
ripoti mpya, UNICEF inasema kuwa mamia ya shule zimeshambuliwa ,
kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumua kwa kipindi
cha miaka sita.
Shule nyingi katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria zimegeuka kuwa kambi za wakimbizi.
Nchini Nigeria kwenyewe wanamgambo hao waliwaua karibu walimu 600.
Katika taifa jirani la Cameroon ni moja tu kati ya shule 100 zilizofungwa mwaka uliopita ambayo imefunguliwa.
Umoja wa mataifa una hofu kuwa huenda watoto hao wakaacha kwenda shule kabisa katika maeneo hayo. Kufikia sasa watu 17,000 wameuawa huku takriban wakaazi milioni 2 wakilazimika kutoroka makwao.
Licha ya amri ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu
Buharikwa makamanda wake wa jeshi kuzima mashambulizi ya Boko Haram
,kundi hilo bado linaendelea kuwaua watu katika ukanda wa Magharibi mwa
Afrika.
Kufikia sasa watu 17,000 wameuawa huku takriban wakaazi milioni 2 wakilazimika kutoroka makwao.
Shule nyingi katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria zimegeuka kuwa kambi za wakimbizi. UNICEF inasema kuwa mamia ya shule zimeshambuliwa ,
kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumua kwa kipindi
cha miaka sita.
Boko Haram ambayo ni tafsriri ya ''elimu ya kisasa
ni haramu'' imekuwa ikilenga shule nchini Nigeria kwa hofu watoto
walioelimika hawafuati masharti na kanuni za dini ya Kiislmu.
Mwaka uliopita kundi hilo liligonga vichwa vya habari kote duniani baada
ya kuwateka nyara wanafunzi 200 wa kike katika mji wa Chibok.
Hadi kufikia sasa wasichana hao wanafunzi hawajulikani waliKO.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments