Tanzania ni moja kati ya nchi
zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya
mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara
hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa
ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa
ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya
kuathiriwa na vijidudu vingine.
Tanzania na Nigeria ndizo nchi
pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye maabara ya aina hii ambayo
itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na
Burundi. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa
magonjwa ya binadamu, NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii
ina umuhimu kwa kuwa itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na
haraka zaidi, hata katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa. Changamoto ambayo ilionekana wakati wa mlipuko wa
ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi ni wahudumu kutofika kwa urahisi
kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi wa haraka kutokana na umbali na
miundo mbinu mibovu.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments