.

.

MAWAKILI WA BESIGYE KWENDA MAHAKAMANI ,NIMGOMBEA WA URAIS NCHINI UGANDA KWA TIKETI YA FDC

ZePLAN | 04:20:00 | 0 comments

Besigye
Mawakili kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye wamesema watawasilisha kesi mahakamni leo kulalamikia kuendelea kuzuiliwa kwake an polisi.

Alikamatwa alipokuwa katika makao makuu ya chama chake cha FDC Ijumaa, siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo, na akarejeshwa kwake nyumbani baadaye jioni.

Amekuwa akikamatwa kila anapojaribu kuondoka nyumbani kwake na kisha kurejeshwa baadaye jioni.

Polisi wamekuwa wakizingira nyumba yake na kuwazuia watu kuingia.

Chama hicho kimepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Jumamosi ambapo Rais Museveni alitangazwa mshindi.

Mawakili wake pia wanatafakari uwezekano wa kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo hayo ya urais.

Bw Besigye amelalamika vikali kutokana na hatua ya kuzuiliwa nyumbani na maafisa wa usalama.

Ujumbe uliopakiwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, baada yake kurejeshwa nyumbani kwake Alhamisi, unasema: “Jioni hii, najihisi kama naweza kuwa ‘gaidi’ halisi.”

Amesema iwapo kuna sababu ya kumzuilia, basi anafaa kuzuiliwa gerezani au eneo lililotangazwa kuwa seli la sivyo aachiliwe huru na kuruhusiwa kutembea.

Alhamisi alikamatwa alipokuwa akijaribu kuelekea afisi za FDC eneo la Najjanankumbi mwendo wa saa tano mchana na akaachiliwa huru saa tatu usiku.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments