.

.

MBWANA SAMMATTA AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI UBELGIJI KAMA KAWAIDA YAKE

ZePLAN | 17:16:00 | 0 comments

Samatta
 Samatta alisema alifurahia sana kufunga bao

Mshambuliaji nyota wa Tanzania Mbwana Ally Samatta amefungua akaunti yake ya mabao Ulaya baada ya kuifungia klabu yake mpya ya KRC Genk bao dhidi ya Club Brugge.

Samatta alifunga bao lake dakika ya 81 na kusaidia klabu hiyo kupata ushindi wa 3-2 baada ya kuingia uwanjani kama nguvu mpya dakika ya 77.

Klabu yake ilikuwa ikiongoza 2-1 wakati huo.
Club Brugge baadaye waliongeza la pili kupitia mchezaji Vanaken dakika ya 83 lakini hawakufanikiwa kufuta uongozi wa Genk, mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Ubelgiji iliyochezewa uwanja wa nyumbani wa KRC Genk wa Cristal Arena, Jumapili.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments