.

.

ALIKO DANGOTE AZIDI KUTUTUMUA POCHI MALI YAKE YAZIDI BILIONI 15.4

ZePLAN | 22:18:00 |

 Dangote Group signs $4 billion deal with China, eyes new markets ...


Mtu tajiri barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote amepanda katika watu matajiri katika orodha ya Forbes ya watu mabilionea ,huku mali yake ikiongezeka na kufikia dola bilioni 15.4.

Bwana Dangote ameorodheshwa wa 51 duniani ukilinganisha na nafasi ya 67 mwaka 2015 wakati gazeti hilo la Forbes lilipoiweka mali yake kufikia dola bilioni 14.7.

Ni mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement ,ikiwa ndio kampuni kubwa katika uzalishaji wa simiti barani Afrika.


Mtu wa pili kwa utajiri barani Afrika ni raia mwengine wa Nigeria ,Mike Adenua ambaye ana thamani ya dola biloni 10,huku raia wa Afrika Kusini Nicky Oppeheimer akiwa katika nafasi ya tatu na mali yenye thamani ya dola bilioni 6.6.

Gazeti hilo linamuweka Adenua ambaye alitajirika kutokana na mafuta na kampuni za mawasiliano katika nafasi ya 103 katika orodha ya mabilionea duniani huku Openheimer akiwa nafasi ya 103.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!