.

.

RWANDA :WALIO MUASI RAIS PAUL KAGAME KUKIONA CHAMTEMA KUNI

ZePLAN | 22:22:00 |

Rais wa Rwanda  Paul Kagame
Aliyekuwa mlinzi wa rais Paul Kagame na mshirika wake wanakabiliwa na hukumu ya miaka 22 gerezani kwa kupanga njama dhidi ya kiongozi huyo wa Rwanda.

Afisi ya kiongozi wa mashtaka nchini Rwanda imeitaka mahakama iwahukumu kifungo cha miaka 22 kanali Tom Byabagamba aliyeiongoza kikosi cha kumlinda rais , na brigedia mstaafu jenerali Frank Rusagara kwa makosa ya kuchochea uma dhidi ya rais Kagame.

Maafisa hao wakuu jeshini walikamatwa mnamo mwezi Agosti 2014.

Wamekanusha madai dhidi yao.
Kiongozi huyo wa Mashtaka alisema mahakamani kuwa Brig-jenerali Rusagara alisikika akiituhumu serikali ya Rwanda kuwa "taifa linalotawaliwa kiimla na kuwa ni taifa lililofeli'
Aidha alidai kuwa '' bwana Kagame ni kiongozi wa kiimla''.

kanali Byabagamba anatuhumiwa kwa kudai kuwa kundi la wapiganaji wa kihutu wa FDLR, waliotekeleza mashambulizi mengi katika taifa jirani la jamhuri ya Congo hawakuwa tishio kwa Rwanda.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!