AMCHOMA MWENZAKE KISU MPAKA KIFO CHANZO KIKIWA NI MABISHANO NI NANI BORA KATI YA RONALDO NA MESSI INDIA
Ubishi wa Messi na Ronaldo wasababisha mauti |
Polisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga kisu rafikiye waliyekosana kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.
Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.Inspekta mkuu wa polisi Kiran Kabadi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa Michael Chukwuma, 21 ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai.
Yamkini yeye na mwenzake walianza gumzo kuhusu mchezaji bora katika kitongoji kimoja cha Nallasopara.
Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
''Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.'' alisema Inspekta hyo wa Polisi.
Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika, aliongezea Kabadi.
Category:
0 comments