.

.

SOMALIA: BOMU LILILOKUWA KATIKA KIPAKATISHI (LAPTOP) LALIPUKA NA KUUWA HUKU MAAFISA POLISI WAWILI WAKIJERUHIWA

ZePLAN | 04:59:00 | 0 comments

   
Bomu la Laptop lalipuka Somalia 
                                                    
Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.
Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
Mtu aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje ya Mogadishu.
               
Mwezi uliopita,kundi  la Al-Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.

Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).

''Afisa wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2 yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa (printer)

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments