.

.

DK JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KATIBU MPYA ATAKAE KAMATA NAFASI YA OMBENI SEFUE

ZePLAN | 14:44:00 | 0 comments

Rais John Pombe Magufuli
Mhandisi John William Kijazi ameteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi nchini Tanzania.
 
Kabla ya kuteuliwa leo Mhandisi Kijazi alikuwa anahudumu kama balozi wa Tanzania nchini India ambapo majuzi tu alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi raia wa Tanzania wanapata usalama kufuatia shambulizi dhidi ya mmoja wao.

Katika taarifa fupi kutoka kwa ikulu ya rais John Pombe Magufuli Balozi huyo anaanza kazi mara moja.

Mhandisi Kijazi anachukua nafasi iliyowachwa wazi baada ya kuondolewa Balozi Ombeni Sefue.

Haijulikani kwanini balozi Sefue ameondolewa katika wadhfa huo ila taarifa hiyo ya ikulu iliyotiwa sahihi na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa inasema kuwa Sefue atapewa majukumu mengine.Mtazame Rais J.P.Magufuli hapa...

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments