.

.

MKUTANO WA OBAMA NA WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU WAKATISHWA GHAFLA

ZePLAN | 00:38:00 | 0 comments

Ikulu ya Marekani imesema mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Barack Obama wa Marekani umefutwa katika mazingira ya utata.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
 
Imeelezwa kuwa Netanyahu alitakiwa kukutana na Rais Obama ndani ya mwezi huu.

Msemaji wa Ikulu ya Rais Obama amesema kuwa wameshtushwa na hatua ya Netanyahu kuamua kukatisha ghafla ziara yake na kwamba taarifa hizo wamezisikia kupitia vyombo vya habari.

Amesema kuwa madai ya kwamba mkutano huo umeshindikana kutoka na kukosekana kwa maandalizi si kweli.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments