RAIS WA MEXICO ENRIQUE PENA NIETO AMFANANISHA DONALD TRUMP NA MADIKTETA
Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na pia kwenye kura za maoni chama cha Republican
Rais wa Mexico
Enrique Pena Nieto amesema lugha anayotumia mgombea urais wa chama cha
Republican Donald Trump ndiyo iliyotumiwa na madikteta Adolf Hitler na
Benito Mussolini.
Benito Mussolini |
Kiongozi huyo amesema matamshi ya Trump yameathiri uhusiano kati ya Mexico na Marekani, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Alipoulizwa kuhusu Trump, Pena Nieto alisema mambo ambayo mgombea huyo amekuwa akiyafanya na kuyapendekeza “yamewahi kusababisha maafa makubwa katika historia.”
Adolf Hitler |
“Hivyo ndiyo Mussolini alijitokeza na ndivyo Hitler alivyojitokeza,” amesema Pena Nieto.
Bw Pena Nieto alikuwa hajazungumza moja kwa moja kumhusu Bw Trump ambaye ameahidi kujenga ua kati ya Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kutoka nchi hiyo wasiingie Marekani.
Bw Trump alisema wahamiaji hao huingiza mihadarati na uhalifu Marekani na kwamba ni “wabakaji”.
Marais wa zamani Vicente Fox na Felipe Calderon pia wamemtaja Hitler wakimzungumzia Trump.
Bw Pena Nieto amesema kamwe Mexico haitafadhili mpango wa kujenga ukuta mpakani kama alivyopendekeza Bw Trump.
Lakini ameeleza matumaini kwamba wapiga kura watamkataa Bw Trump.
Category:
0 comments