.

.

RAIS OBAMA AMTOA HOFU RAIS WA CUBA RAUL CASTROL KUWA ASIOGOPE MAREKANI

ZePLAN | 03:45:00 | 0 comments

CubaRais wa marekani Barack Obama 
 

Rais wa Marekani Barack Obama ameeleza matumaini yake kwamba hali ya Cuba itaimarika, kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga.

Kiongozi huyo wa Marekani, ambaye ndiye wa kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo kutoka ukumbi wa Grand Theatre mjini Havana.

Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama.

Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa “usemi wa watu wa Cuba”.
Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani na Cuba kuacha nyuma yaliyopita na kusonga mbele “kama marafiki na majirani na kama familia, pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi.
 
ObamaJumatatu, viongozi hao walijibizana kwenye kikao na wanahabari
Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya kifalsafa na kujieleza sio kwa kupinga Marekani bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa Cuba.

"Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na Wacuba ni Wacuba,” alisema.

Aidha, amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana na raia wa Cuba.

Ni Bunge la Congress pekee linaloweza kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Rais Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu kwa kuungana na Rais Castro kutazama mechi ya besiboli uwanja wa Latinoamericano mjini Havana.
Tampa Bay Rays waliilaza timu ya taifa ya Cuba 4-1.

Baada ya kuondoka Cuba,Rais Obama ameelekea Argentina siku ambayo inalingana na maadhimisho ya miaka 40 tangu kutokea kwa mapinduzi yaliyoingiza mamlakani utawala dhalimu wa kijeshi.

Baadhi ya makundi yanapanga maandamano kushutumu Marekani ambayo inadaiwa kusaidia jeshi wakati wa mapinduzi hayo ya 1976.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments