RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA KUIONGEZEA VIKWAZO NCHI YA KOREA KASKAZINI
Rais wa Marekani
Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada
ya taifa hilo kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi
majuzi.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii
ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu za nyuklia” zinazotekelezwa
na Korea Kaskazini.
Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea
Kaskazini ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani katika juhudi
za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.
Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru mwanafunzi huyo mara moja.
Category:
0 comments