TRUMP ATABIRI KUHUSU KUZUKA KWA FUJO NCHINI MAREKANI
Trump ameshindwa katika mchujo jimbo la Ohio
Mfanyabiashara
tajiri Marekani Donald Trump, amesema anafikiri kutatokea fujo iwapo
ataongoza kwa wajumbe kisha chama chake cha Republican kitakosa
kumuidhinisha awanie urais.
Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican, ambao hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa kuidhinisha wagombea Julai.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders katika majimbo manne yaliyofanya mchujo Jumanne.
Category:

0 comments