.

.

RAIS WA TANZANIA ATOBOA JIPU JINGINE BOT AKUTA MAJINA YA WAFANYAKAZI HEWA ATOA KAULI NZITO TAZAMA VIDEO HAPA

ZePLAN | 23:24:00 | 0 comments

Rais Magufuli akiwaonyesha wakuu wa BOT majina ya wafanyakati hewa ambao uongozi umekili kufanya makosa na kuahidi watarekebisha mara moja kwa kuyaondoa kwenye vitabu vya BOT.

Rais amewaamuru wayaondoe mara moja ili pesa zitumike kulipa wafanyakazi wanaostahili kulipa kama wafanyakazi wa BOT.

Rais amesitikishwa na uzembe na pia wizi unaofanyika BOT kwa njia za udanganyifu.



Angalizo:

Baadhi ya maneno ya Rais Magufuli wakati akiongea na wananchi wa Arusha na hali iliokutwa BOT

‘’Tanzania hii, ilikuwa shamba la bibi, watu walikuwa wanafanya ya ovyo. Ninaposema ya ovyo ni ya ovyo kweli, mimi nipo serikalini, lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20, ninayajua. Ninaposema ya ovyo, ndugu zangu naomba mniamini.
“Mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama. Ukikosa madawa hospitalini hata ukiwa Chadema utakosa tu, hata ukiwa CCM unaimba kila siku CCM oyeee, utakosa tu madawa. Kwa hiyo hatua tunazotaka kuzichukua ni kwa wananchi wote bila kujali itikadi zao.
“Tumefika katika wakati huu, ni lazima patokee mmoja wa kuyafanya. Na ndiyo maana siku zote nimekuwa nikiwaeleza. Ndugu zangu mimi nimeamua kuwa sadaka ya Watanzania. Kazi hii ni ngumu, ni ya ajabu. Kila mmoja anajitahidi haya tunayoyafanya tusiyafanye, lakini nawashukurui mnaendelea kuniombea. Ndiyo maana niko hapa. Endeleeni kutuombea lengo letu ni la kuwasaidia ninyi. Ni lazima tufanye’’.

Tazama video kwa kubonyeza hapo chini ...........

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments