RAIS WA VIETTNAM KUJA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI TANZANIA
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano cha Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga akimkaribisha
Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuzungumza na
waandishi wa habari(hawapo pichani). Kulia ni Waziri Balozi Dkt.
Mahiga.Picha na Wizara.
Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishiwa habari kuhusu
ujio wa rais wa Vietnam hapa nchini kushoto ni Mindi Kasiga Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano cha Waziri wa Mambo ya Nje.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Hussein Makame-MAELEZO
RAIS wa
Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya
ziara ya kikazi nchini Tanzania Machi 9 mwaka huu ikiwa ni ziara yake ya
kwanza Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema lengo la ziara hiyo ni kukuza
uhusiano baina ya Tanzania na Vietnam ambao umedumu kwa zaidi ya miaka
50 sasa.
Alisema
Rais Sang atawasili siku ya Jumatano na ataanza shughuli mbalimbali
Alhamisi kwa kufanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam.
Baada ya
kukutana na Rais Dkt. Magufuli, Rais Sang atasaini mkataba kuhusu
masuala ya kodi na baadaye atafungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa
kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam.
Alisema
lengo la mkataba huo ni kuchochea biashara baina ya Tanzania na Vietnam
ambapo wafanyabiashara wa nchi hizo hawatatozwa kodi mara mbili kwa
biashara na uwekezaji watakaoufanya.
Rais Sang
pia atapata fursa ya kukutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutembelea eneo la
EPZ la Ubungo.
Akiwa
EPZA Rais Sang atatembelea viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa
zinazouzwa kuuza nje ya nchi kabla ya kuhudhuria mkutano wa biashara na
uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere.
Waziri
Balozi Mahiga alisema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na
taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
Katika
ziara hiyo pia atapata fursa ya kuzungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein.
Kwa
mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Rais Sang pia atahudhuria dhifa ya
Kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
Kabla ya
kuondoka nchini Rais Sang atatembelea moja ya mbuga za wanyama zilizopo
nchini ili kujionea vivutio vya kitalii vilivyopo kwenye mbuga hiyo na
kuwashawishi raia wa Vietnam kuja kutalii nchini.
Rais
Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4
wanaoshughulika na sekta za Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya Viwanda
na Biashara. Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara
30 kutoka Vietnam.
Baada ya kuondoka nchini siku ya Ijumaa, Rais Sang anatarajiwa kwenda nchini Msumbiji kwa ziara ya kikazi.
Rais Sang
wa Vietnam amezaliwa tarehe 21 January 1949 katika Jimbo la Long An
nchini Vietnam na 25 Julai 2011 apochaguliwa na Bunge la Vietnam kuwa
Rais wa Vietnam.
TAZAMA VIDEO HAPA ........................
Category:
0 comments