.

.

TEMBO ALIE POTEA TAKRIBANI MIONGO MIWILI AREJEA KWAO SOMALIA

ZePLAN | 08:21:00 | 0 comments

               
Ndovu mmoja kwa jina Morgan amefanikiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Somalia mwezi huu, na kuwa mara ya kwanza ndovu huyo kuonekana nchini humo tangu miaka 20 iliyopita.
Ndovu huyo kwa jina Morgan aliye na umri wa takriban miaka 30, alifungiwa kifaa ya kufuatilia mienendo yake mwezi Disemba katika eneo la Tana River pwani mwa kenya, kati kati ya mwezi Februari kabla ya kuanza safari isiyotarajiwa kuelekea nchini Somalia na kufanikiwa kuwasili mpakani wiki tatu baadaye.
 
   Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuwa lenye usalama.                
Safari yake imewashangaza watunza mazingira ambao wanasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa ndovu huyo alikumbuka njia za zamani baada ya miongo kadha ya kuondoka Somalia kutokana na mapigano.
Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuboreka kiusalama na ikiwa hali itakuwa shwari kusini mwa Somalia, basi ndovu waishio uhamishoni watarudi nyumbani.
 
Kutoka ene la Tana River Morgan alitembea umbali wa kilomita ishirini usiku wa kwanza kabla ya kujificha ndani ya msitu mkubwa na kuendelea na safari siku iliyofuata . Alirudia mtindo huo kwa siku 18.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments