WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AOMBA RADHI JAMII YA WA OROMO
Katika taarifa ya moja kwa moja kupitia televisheni amedai kuwa watu wa itikadi kali wamejaribu kupanda mbegu za chuki baina ya jamii tofauti ambazo zimeishi kwa amani kwa miaka mingi
nchini humo na kuongeza kuwa serikali yake itawachukulia hatua
Maandamano yamekuwa yakiendelea dhidi ya hatua ya utawala kutaka kufanya upanuzi wa mji wa mkuu Addis Ababa ambao ungemegua baadhi ya maeneo ya wanavijiji wa Oromo, japo hatua hiyo ilisitishwa tangu mwezi January.
Wachambuzi wanasema japo Oromo ndio jamii kubwa zaidi nchini Ethiopia, wanalalamikia kile wanachokiita ukandamizwaji ukiwemo wa lugha yao ya Amharic.
Category:
0 comments