ZIMBABWE KULIPA FIDIA WAKULIMA WAZUNGU WALIOPOTEZA ARDHI NA MALI WAKATI WA UKOLONI
Taarifa kutoka Zimbabwe zinasema serikali inafanya mipango ya
kuwalipa wakulima wazungu waliopoteza ardhi wakati wa uvamizi ulioungwa
mkono na serikali miaka 16 iliyopita.
Shirika la habari la
The Bloomberg linasema wizara ya fedha ya Zimbabwe imetoa taarifa
ikieleza kuwa wakulima hao watapokea fedha kufidia hasara waliopata ya
ardhi na mali.
Waandishi nchini humo wanasema iwapo hatua hiyo
itathibitishwa, itakuwa sawa na kwenda kinyume na kauli ya rais Mugabe
kupinga malipo yoyote kwa ardhi hiyo.
Mugabe amesisitiza katika
siku za nyuma kuwa wakulima hao hawapaswi kulipwa kwasababu ardhi hiyo
iliibiwa kutoka kwa Waafrika wakati wa utawala wa mkoloni.
Uvamizi
huo ulilenga mashamba ya tumbaku, zao lililouzwa kwa wingi kwa wakati
mmoj kutoka Zimbabwe, na hilo likasababisha ukame mkubwa kati nchi hiyo
iliyokuwa muuzaji wa pili kwa ukubwa Afrika wa mahindi.
Zimbabwe inajaribu kuurudisha uhusiano na shirika la fedha la kimataifa IMF na taasisi nyengine za fedha duniani.
Category:
0 comments