.

.

ALIEKUWA MLINZI WA GADDAFI AUMWA NA NYOKA AKIPATA HAJA MSITUNI

ZePLAN | 00:52:00 | 0 comments

 

Saad Gaddafi Aliyekuwa mlinzi wa mwana wa Gaddafi ambaye baadaye alifanya kazi katika baa moja nchini Australia ameumwa na nyoka alipokuwa akifanya haja ndogo msituni.

Raia huyo wa Australia Gary Peters alikuwa mlinzi wa Saad Gaddafi ,mwana wa aliyekuwa rais wa Libya Muamar Gaddafi lakini kwa sasa anafanya kazi katika kilabu moja.

Raia huyo mwenye umri wa miaka 52 alikuwa akinywa vinywaji pamoja na marafikize baada ya kazi siku ya Jumatano wakati alipotoka ili kwenda haja ndogo.

Bwana Peter alikuwa amemaliza kufanya haja ndogo wakati nyoka huyo alipomng'ata kifundo cha mguu.
Aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi
Anasema aliona sumu ikimwagika kutoka kwa mguu wake na kuhofia kwamba angefariki.
''Nilimwagiwa sumu kidogo .Iwapo ningemwagiwa nyingi pengine ningekuwa katika jeneza alisema,'' Peters.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments