PANYA WAILAZIMISHA UINGEREZA KUKODISHA PAKA
Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka
Je unampenda paka ?
Awe ni paka wa nyumbani ama yule paka wa mwituni na wanyama wote katika jamii ya pakaa kama vile simba,ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana kwa mwanadamu.Video za paka ni maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii.
Amini usiamini afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Kituo cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au maadui, katika makao hayo yake mapya katika afisi ya wizara ya nchi za kigeni.
Category:
0 comments