Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.
Spika
wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo
kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom
Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Spika Baleka
Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais
Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi
mabaya ya madaraka yake.
Spika Baleka Mbete
Siku
ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume
na katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati
nyumba yake ya binafsi.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani
baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika
kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa
zilizotumiwa. Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atatakikana kuzirejesha.
Rais Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya kikatiba uliompata na
hatia na akaapa kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla
kama ilivyoamua mahakama.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments