.

.

WHATSAPP KULINDA MAWASILIANO YA WATEJA WAKE

ZePLAN | 07:04:00 | 0 comments

Image result for whatsapp images Huduma ya WhatsApp

Huduma ya ujumbe Whatsapp imetangaza kuwa itayalinda mawasiliano ya wateja wake kuanzia hapo jana siku ya Jumanne.

Huku ulinzi ukiwekwa mwanzo na mwisho wa ujumbe ,ujumbe uharibiwa wakati unapotoka katika simu ya anayeutuma na unaweza kusomwa pekee na anayeupokea.

Hatua hiyo utaufanya ujumbe huo kutosomeka iwapo muhalifu ama hata maafisa wa polisi wanajaribu kuingilia simu simu bila idhini.

WhatsApp ambayo ina wateja zaidi ya bilioni moja duniani imesema kuwa uhamisho wa faili pamoja na sauti pia zitalindwa.

Huduma hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Facebok imesema kuwa ulinzi wa mawasiliano ya faragha ni miongoni mwa malengo yake.

Ulinzi huo uliathiriwa wakati shirika la Marekani la FBI lilipotaka kampuni ya Apple kuisadia kuchukua data katika simu moja ya iphone iliotumiwa na muuaji Syed Farook.

Whatsapp ilisema:Wazo hilo ni rahisi, unapotuma ujumbe mtu pekee anayeweza kuusoma ni mtu ama kundi la mawasiliano ambalo umelitumia ujumbe huo.

Hakuna mtu anayeweza kuusoma ujumbe huo hata kama ni wahalifu wa mitandaoni ama hata serikali.hata sisi hatuwezi kuusoma.

Watumiaji wapya wa huduma hiyo waliarifiwa kuhsu mabadiliko hayo wakati wanapotuma ujumbe siku ya Jumanne.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments