.

.

BASATA WATOA TAMKO ZITO JUU YA SNURA MUSHI NA NYIMBO YAKE YA CHURA

ZePLAN | 01:16:00 | 0 comments


  Picha juu Snura 
               
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wimbo na kanda ya video ya muziki kwa jina CHURA wa msanii Snura Mushi kuchezwa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi pale msanii huyo atakapoufanyia marekebisho wimbo huo.

Vilevile Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamuziki huyo hadi pale atakaposajili kazi zake katika baraza la taifa la sanaa BASATA.
Hatua hiyo inafuatia maudhui ya utengenezwaji wa video hiyo ambayo serikali inasema inakiuka maadili ya raia wa Tanzania.

Serikali imesema kuwa kazi ya mwanamuziki huyo inadhalilisha tasnia ya muziki nchini Tanzania.
Hata hvyo Snura mushi bado hajatambulika kama msanii kamili ambae anatambulika na balaza hilo kutokana nakile kinachodaiwa uwa hajajisajili BASATA na taarifa zake hazipo kwenye baraza hilo.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments