.

.

WABUNGE SOUTH AFRIKA WATIANA MAKONDE

ZePLAN | 01:23:00 | 0 comments


Picha juu Wabunge wa EFF                 
Wabunge nchini Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni tayari kulihutubia bunge hilo.

Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani.
Hata hivyo ujio wake uliwakera sana wabunge wa chama cha upinzani Economic Freedom Fighters (EFF).

Wabunge hao chini ya kiongozi wao Julius Malema walipiga mayowe na kumtupia matusi bw Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru wabunge hao wa EFF kuondolewa nje.
Ijumaa iliyopita mahakama ya juu ya Afrika Kusini iliamua kuwa rais Zuma anapaswa kufikishwa kizimbani kufuatia kesi za ufisadi dhidi yake.
Picha juu Zuma                 
Kesi hiyo inahusiana na ufisadi uliotokea katika ununuzi wa silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola mwaka wa 1999.
Zuma amekanusha madai yote dhidi yake.
Anatarajiwa kukamilisha hatamu yake mwaka wa 2019.

Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa msumari wa moto kwa kidonda cha Zuma ambaye mwezi uliopita alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake alipokaidi amri yakulipa pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya Nkandla.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments