Meli hiyo iitwayo Adonia, imebeba abiria wapatao mia saba,imeng’oa nanga kutoka katika bandari ya Miami na inatarajiwa kufika tamati ya safari yake Jumatatu ijayo.

Cuba na Marekani zimerejesha uhusiano baina yao wa kidplomasia mwaka wa jana, ingawaje vita baridi iliyokuwa baina ya nchi hizo ilisababisha hali kibiashara kati yao kuwa ya kusua sua na bado hali si shwari mpaka sasa.

Safari hiyo ya kihostoria kwa njia ya maji imepiga hatua moja kubwa mbele katika kuuimarisha uhusiano huo wa kidlomasia na hii ni baada ya serikari ya Cuba kukubali kuondoa marufuku ya raia wake kuingia nchini Marekani ama kutumia maji kama njia ya usafiri kuingia nchini humo.
Adonia-500x325Picha juu Meli kubwa ya Marekani Adonia, ikiwa na abiria mia saba ndani yake ikielekea Cuba.