SOMALIA YAPIGA MARUFUKU NDEGE KENYA ZA MIRUNGI
Serikali ya Somalia imesitisha kwa ndege zote zinazoingiza miraa kutoka taifa jirani la Kenya.
Biashara hiyo ina thamani ya mamia ya mamilioni ya madola kila mwaka.
Waziri
wa maswala ya anga nchini Somalia Ali Ahmed Jama Jangali,amesema kuwa
marufuku hiyo itaanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini hakutoa maelezo
zaidi.
Miraa ni maarufu sana nchini Somalia ,ambapo hutafunwa kwa saa kadhaa na hutumika kusisimua mwili .
Haikuzwi nchini Somalia.
Miraa hutumika na imepigwa marufuku nchini Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya.
Category:
0 comments