SENEGAL YASEMA JAMEE LAZIMA ANG'ATUKE MADARAKANI
Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz yuko nchini Gambia kwa kile kilichotajwa kuwa ni juhudi za mwisho za kumshauri bwana Jammeh kuachia madaraka kwa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal.
Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
Category:
0 comments