.

.

MBWA AMEZA KISU CHA SENTIMITA 20

ZePLAN | 22:57:00 | 0 comments

Macie kwa sasa anaendelea kupata nafuu                           

               
Mbwa ambaye alimeza kisu cha urefu wa sentimita 20 anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mbwa huyo wa umri wa wiki 12 kwa jina Macie, alikimbizwa kwa daktari wa mifugo kwa huduma ya dharura baada ya kuanza kukohoa.

Mwenye mbwa huyo anasema alidhani kuwa alikuwa amemeza kifaa cha kuchezea cha watoto, lakini X ray baadaye ilionyesha picha ya kisu kikuwa tumboni.

Daktari ambaye amekuwa akimtunza mbwa huyo tangu afanyiwe upasuaji anasema ana habati sana kuwa hai.

Mwenye mbwa huyo kutoka Glasgow alikuwa amempoteza mbwa wake mwingine kutokana na ugonjwa wa saratani.

Siku moja baada ya kufanyiwa upusuaji alionekana mchangamfu. Mbwa huyo amekuwa akirudishwa kwa daktari kufanyiwa ukaguzi kwa muda wa wiki mbili na sasa anaendelea kupata nafuu.

Picha za X-ray zilionyesha kisu ndani ya tumbo

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments