COLOMBIA:RAIS NCHINI HUMO ATANGAZA HALI YA TAHADHARI
Juan Manuel Santos amesema serikali inakusanya $ milioni 13.9 zitakazosaidia kukabiliana na masuala ya kibinaadamu.Wakati huo huo mazishi ya kwanza ya wahanga 262 waliouawa katika maporomoko ya Jumamosi yamefanyika. Lakini bado jitihada za kutafuta manusura zinaendelea.
Shirika la msalaba mwekundu limeliambia shirika la habari la AFP kwamba bado wana muda katika saa 72 za kwanza baada ya mkasa na wanatumai kupata manusura. Hatahivyo matumaini yanafifia miongoni mwa wakaazi wanaotafuta jamaa zao waliosombwa katika udongo, mawe na kifusi vinavyotokana na maporomoko hayo yalioukumba mji huo uliopo kusini magharibi mapema Jumamosi.
Rais Santos ameahidi uwekezaji zaidi katika mji wa Mocoa zaidi ya ilivyokuwa awali, na kumkabidhi mamlaka waziri wa ulinzi Luis Carlos Villegas kuusimamia mji huo.
.
Category:
0 comments