SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AMUAPISHA MKE WA RAIS MSTAAFU BUNGENI LEO

Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo amemuapisha mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Rashid Kikwete kuwa mbunge wa Bunge wa kuteuliwa.Mh.Salma aliandamana na mumewe rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye uwepo wake ulisababisha kelele za shamra shamra hoi hoi na nderemo kutoka kwa wabunge wakisema kwa sauti 'tumekumiss tumekumiss wakimshabikia Rais huyo mstaafu [pamoja na familia yake iliokuwepo hapo bungeni.
kurasa ya twitter ya Rais huyo mstaafu ilithibitisha uwepo wake pia katika tukio hilo adhwimu la uwapishaji wa mkewe bibi Salma Kikwete

Huu ni mkutano wa saba wa bunge la Tanzania ukiwa umeanza kikao chake cha kwanza cha mkutano wa bajeti hii leo.
Mama Salma kama anavyotambulika na wengi nchini ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.
Category:
0 comments