.

.

Chanjo ya malaria kwa watoto yatolewa

ZePLAN | 01:19:00 | 0 comments

Hatua za mwisho za majaribio za chanjo dhidi
ya Malaria, ya kwanza kufikia hatua hii inaleta
matumaini kuwa itawalinda mamilioni ya Watoto
dhidi ya Malaria.
Lakini Majaribio kwa watoto 16,000 kutoka nchi
saba za Afrika yameonyesha kuwa kuna mipaka
katika matumizi ya dawa hizo na chanjo haifanyi
kazi kwa watoto wachanga.
Baada ya Watoto kufikia umri wa miezi 5-17
walipewa dozi tatu za chanjo, Kinga ilifanya kazi
mwilini kwa kiasi cha 45%.
Lakini wataalam wanasema hatua ya kuifikisha
chanjo katika hatua hiyo ni kupiga hatua kubwa.
Data zilizochapishwa katika jarida moja la
maswala ya kitabibu zinaonyesha mafanikio ya
chanjo hiyo ni madogo mno kwa vichanga.
Wanasayansi wamekuwa wakifanyia kazi chanjo
hiyo kwa zaidi ya miaka 20, lakini wachunguzi
wa mambo wanaona kuwa bado kazi kubwa
inahitajika.
RTS,S/AS01 ni Chanjo ya kwanza ya Malaria
kufikia hatua za juu za majaribio.
kwa sasa hakuna chanjo yoyote dhidi ya Malaria
iliyopatiwa kibali duniani.
Chanjo hizi zilitolewa katika nchi 11 ikiwemo
Tanzania,Kenya,Burkina Faso,
Gabon,Ghana,Malawi na Msumbiji.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments