.

.

UINGEREZA:Wanawake watia fora kwenye viapo vitakatifu

ZePLAN | 02:33:00 | 0 comments

Idadi ya wanawake wanaokuwa watawa
imeongezeka pakubwa katika kipindi cha miaka
25,kanisa katoliki nchini Uingereza na Wales
limesema.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake
wanaokula viapo vitakatifu imeongezeka mara
tatu katika kipindi cha miaka mitano kutoka
wanawake 15 mwaka 2009 hadi 45 mwaka
uliopita,ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka 1990.
Wanawake 14 walioingia katika utawa mwaka
2014 walikuwa na miaka 30 ama chini yake
,takwimu mpya zinaonyesha.
Kanisa hilo linasema kuwa wanawake
wanajiingiza katika maisha ya kidini kutokana na
pengo la utamaduni kutotiwa maanani.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 1980
takriban wanawake 80 walijiunga na utawa lakini
idadi hiyo ilipungua hadi mwaka 2004 ambapo
wanawake saba pekee walijiunga na utakatifu
huo.
Idadi hiyo imeongezeka katika kipindi cha miaka
10 ambapo ilifika 45 mwaka 2014

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments