UN YAOMBA VITA ISITISHWE
Umoja wa mataifa umetoa wito wa ghasia
zimalizwe katika eneo la Yarmouk, kambi ya
Wapalestina mjini Damascus, ili kuruhusu raia
waondolewe.
Eneo hilo kwa jumla sasa linadhibitiwa na
wapiganaji wa Islamic State, ambao
wanapambana na wanamgambo wa Kipalestina.
Yarmouk ni mahala ambapo tayari wanawake
wanakufa wanapoji-fungua kwa kukosa dawa,
huku watoto pia wakifariki kutokana na njaa.
Sasa mapambano makali yanaendelea barabarani,
watu wamejificha majumbani mwao wakiogopa
kwenda popote.
Category:
0 comments