WACHEZAJI WASHAMBULIWA NA RISASI UTURUKI
Basi la kilabu ya Fenerbahce lilifyatuliwa risasi
na wapiganaji baada ya kilabu hiyo ya Uturuki
kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi kilabu ya
Rizespor.
Dereva wa basi hilo alipelekwa hospitalini lakini
hakuna mchezaji aliyejeruhiwa wakati wa
shambulio hilo ambalo lilitokea wakati
walipokuwa wakielekea katika uwanja wa ndege
wa Trabzon.
Waziri mkuu wa taifa hilo Ahmet Davutoglu
amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
Basi la kilabu ya fenerbahce nchini Uturuki
Shrikisho la soka nchini Uturuki lilishtumu
shambulio hilo huku katibu mkuu wa kilabu hiyo
Mahmut Uslu akisema kuwa kitendo hicho ni cha
makosa.
''Tulikuja hapa kucheza soka'', alisema Uslu
ambaye alikuwa katika basi hilo wakati wa
shambulio hilo.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako
Picha chini muonekano wa basi hilo baada ya kushambuliwa
Category:
0 comments