.

.

Takwimu inaonyesha wanaume wengi hupigwa na wake zao nchini Kenya

ZePLAN | 15:06:00 | 0 comments

Mmoja kati ya wanaume 10 wa Kenya amepigwa
na mkewe ama mpenziwe kulingana na utafiti wa
kiafya.
Wanaume walio kati ya umri wa miaka 20 hadi 24
ambao ni asilimia 11.7 wamevumilia unyanyasaji
huo na wamekuwa wakifuatiwa kwa karibu na
wale walio na kati ya umri wa miaka 40 na 49
wakiwa asilimia 9.8.
Wale walio kati ya miaka 30 na 39 waliripoti visa
vichache huku asilimia 7.1 wakisema kuwa
walinyanyaswa kulingana na utafiti huo wa
mwaka 2014.
Wanaume waliopewa talaka ama hata kutengana
na wake zao waliriporti visa vya juu vya
unyanyasaji.
Walifuatiwa na wanaume ambao wameoa zaidi ya
mara moja.
Ni asilimia 7.1 ya wanaume ambao wanaishi na
wake zao ambao wameripoti visa vya kupigwa.
Wale ambao wameoa mara moja walikuwa na
visa vichache ikilinganishwa na wale ambao
wameolewa mara mbili ama hata zaidi.
Wanaume ambao hawakukamilisha elimu ya
msingi waliripoti visa vingi vya unyanyasaji
wakifuatiwa na wale ambao wamekamilisha
masomo ya msingi na yale ya shule za upili..

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments