.

.

MICHEZO

ZePLAN | 13:57:00 | 0 comments

Arsenal yaibuka kidedea kwa kuichabanga Liverpool mabao 4 wakati Liverpool wakiambulia bao1 lakufutia machozi

Arsenal imeimarisha uongozi wao wa kushiriki
katika mechi za vilabu bingwa barani Ulaya
baada ya kuicharaza Liverpool mabao 4-1 katika
uwanja wa Emirates.
The Gunners iliweka wazi lengo lao la kuchukua
pointi zote tatu baada ya kufunga mabao matatu
ya haraka katika dakika nane za mwisho za
kipindi cha kwanza kupitia Hector Bellerin,Mesut
Ozil,na Alexi Sanchez huku mshambuliaji Olivier
Giroud akipiga msumari wa mwisho wa jeneza la
Liverpool alipofunga bao la nne katika kipindi cha
pili.
Arsenal
Wakati huohuo Manchester United imeishinda
Aston Villa mabao 3-1 na kupanda hadi nafasi ya
tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Kipa wa Aston Villa Brad Guzan alipangua
mkwaju uliopigwa na mlinzi Marcos Rojo lakini
alifungwa na Anders Herrera baada ya kazi nzuri
kutoka kwa Daley Blind.
wachezaji wa Liverpool
Wayne Rooney aliongeza bao la pili alipofunga
katika kona ya mlingoti wa goli.
Hatahivyo Villa walipata bao la kufutia machozi
kupitia mshambuliaji wao Benteke huku Anders
Herrera akifunga udhia.

Kwa maoni na ushauri :
Ochec54@gmail.com

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments