VIJANA WAJIUNGA NA KUNDI LA UGAIDI
Zaidi ya wapiganaji wa kigeni elfu ishirini na
watano kutoka mataifa mia moja walisafiri kwa
nia na malengo ya kujiunga na makundi ya
kijeshi kama al-Qaeda na Islamic State (IS),
taarifa ya umoja wa mataifa imeeleza hayo.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba wapiganaji
wageni ulimwenguni idadi yao imeongezeka
mpaka kufikia asilimia sabini na moja katikati ya
mwaka 2014 na march mwaka huu.
Nchi za Syria na Iraq ndizo nchi zinazolengwa
kwa ukaribu zaidi na ndicho kitovu cha vijana
wanaomaliza mazomo yao na kugeuka kuwa
wenye msimamo mkali wa kidini.
Na pia taarifa hiyo imebainisha kuwa endapo
kundi la IS lingeshindwa nchini Syria na Iraq,sasa
wapiganaji hao kutoka nchi za kigeni
wamesambaa ulimwenguni .
Nalo baraza la usalama la umoja wa mataifa
liliwaomba wataalamu wa masula ya kijeshi miezi
sita iliyopita kuchunguza vitisho vya askari wa
kigeni wanaojiunga na kundi la Is na makundi
mengine ya kigaidi.
Katika ripoti iliyowasilishwa kwenye baraza hilo
mwishoni mwa mwezi uliopita ,na wataalamu
wakaeleza kuwa ongezeko la wapiganaji wa nchi
za kigeni zinazidi kuongezeka kulinganisha na
muongo mmoja uliopita .
Maelfu ya wapiganaji wa kigeni ambao hufanya
safari hadi nchini Syria ,Falme za Kiarabu na Iraq
huko hufanya makao na kufanya kazi na
kumalizia masomo ya elimu ya juu kwa wenye
msimamo mkali kamalivyowahi kutokea kwatika
nchi ya Afghanistan miaka ya 1990 .
Syria na Iraq inasemekana ina makaazi elfu
ishirini na mbili kwa wapiganaji hao wa kigeni ,pia
nchini Afghanistan makaazi elfu sita na mia tano
na maelfu ya makaazi nchini Yemen, Libya,
Pakistan na Somalia.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako
Category:
0 comments