SERIKALI YA SOMALIA YATANGAZA DAU
Serikali ya Somalia imetangaza ruzuku ya dola
milioni moja kwa yeyote atakayeisaidia
kuwakamata viongozi 11 wa Al Shabaab.
Orodha hiyo ya watu 11 wanadaia kuwa viongozi
wa ngazi ya juu ya katika kundi hilo la wapiganaji
wa wa kiislamu wa Al shabaab.
Kiongozi wa kundi hilo la wapiganaji Ahmed Diriye
anaongoza katika orodha hiyo huku Serikali ikitoa
ruzuku ya dola laki mbili u nusu ($250,000) kwa
yeyote atakayetoa habari zitakazofichua aliko.
Kitengo cha wanawake cha Al Shabaab
Jumla ya dola milioni moja zimetengwa katika
hatua hii ambayo inalenga kuchochea umma
kuisaidia serikali hiyo kuitokomeza
kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya
wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa nchini
kenya.
Orodha
Kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi
ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa
nchini kenya
Al Shabaab ambayo imetangaza wazi kushirikiana
na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda wameahidi
kuendelea
kuishambulia Kenya hadi serikali hiyo
itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa wanajeshi wa
muungano wa Afrika .
Kundi hilo linataka Kenya iondoe majeshi yake
nchini Somalia
Majeshi ya Muungano huo inashikilia maeneo
mengi ya mijini kwa ushirikiano na majeshi ya
Serikali ya Somalia huku
kundi hilo la Al Shabaab ikitawala maeneo ya
mashambani kusini mwa taifa hilo ambalo
limekuwa bila serikali kwa zaidi ya miongo miwli
sasa.
Category:
0 comments