.

.

Vatikan yamkata baloz

ZePLAN | 14:40:00 | 0 comments

Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya makao
makuu ya papa mtakatifu ya the Vatican na
Ufaransa kuhusiana na uteuzi wa balozi mpya
wa Ufaransa, mjini Rome.
Rais wa Ufaransa Francois Holland,
amempendekeza muumini mmoja wa kanisa hilo
ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa balozi
wake mjini Vatican.
Lakini utawala wa Vatican umesema uteuzi huo
haukubaliki.
Makao makuu ya papa mjini The Vatican
hayajasema lolote kuhusiana na uteuzi huo ,lakini
ni dhahiri kuwa baadhi ya maafisa wakuu katika
kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa
kuhusiana na waumini wa kanisa hilo ambao ni
wapenzi wa jinsia moja.
Papa alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi
kumhukumu mtu yeyote kwa misingi yoyote.
Makao makuu ya kanisa katoliki ,the Vatican
Serikali ya Ufaransa ilimteua laurent Stefanini
kuwa balozi wake mjini vatican mnamo mwezi
Januari mwaka huu.
Balozi Stefanini mwenye umri wa miaka
55,amekiri hadharani kuwa yeye anashabikia
mapenzi ya jinsia moja na amewahi kufanya kazi
katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa
mshauri wa masuala ya kidini katika wizara ya
mambo ya nje ya ufaransa.
Kwa sasa hakuna upande unaoonekana kuwa
tayari kubadili msimamo wake.
Ufaransa ilhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka
2013 na uamuzi wa The vatican wa kukataa
kumkubali balozi Stefanini huenda ikawa ni
thibitisho la The vatican la kutoidhinisha
msimamo huo wa Ufaransa.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments