UN KUTAFUTA FURSA YA KUKAGUA KAMBI YA WAKIMBIZI
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limetaka kupata fursa ya kuingia katika kambi
ya wakimbizi wa Kipalestina ya Yarmouk mjini
Damascus, Syria.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa ameelezea
hali hiyo katika kambi ya wakimbizi 18,000 kuwa
"kinyume cha ubinadamu".
Hali imezidi kuzorota tangu Aprili Mosi, wakati
wapiganaji wa Islamic State walipofanya
shambulizi.
Wanamgambo wa Kipalestina wanaopingana na
serikali ya Syria na baadhi ya wapiganaji wa Free
Syrian Army wanaongoza mapigano dhidi ya
wanamgambo wa Islamic State.
'Hii lazima ikomeshwe'
Mwenyekiti wa baraza hilo la Usalama la Umoja
wa Mataifa lenye wanachama 15, Dina Kawar,
ambaye ni balozi wa Jordan katika Umoja wa
Mataifa, ametoa wito wa "kuwalinda raia...
Kupata misaada ya kibinadamu na msaada wa
kulinda maisha".
Akiwasilisha ripoti kwenye baraza hilo, Pierre
Krahenbuhl, ambaye ni kutoka shirika la Palestina
la kutoa misaada la Unwra, amesema hali ni ya
kukatisha tamaa zaidi kuliko ilivyokuwa".
Mshirikishe mwenzako
Category:
0 comments