.

.

TANZANIA KUWA KITUO CHA USULUHISHO

ZePLAN | 13:33:00 | 0 comments

Dar es Salaam. Tanzania inatarajia
kuzindua kituo cha kimataifa cha
usuluhishi wa migogoro ya kibiashara
kutokana na kukua kwa sekta ya
uwekezaji ikiwamo mafuta na gesi
nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfre Simbeye alisema kituo hicho
kitazinduliwa Juni mwaka huu na
kitasimamia na kutatua migogoro yote ya kibiashara itakayojitokeza katika kipindi hiki cha ugunduzi wa gesi na mafuta.
Simbeye alisema, kuanzishwa kwa kituo hicho kunatokana na kuongezeka kwa wawekezaji nchini, kuboresha biashara na kuongezeka kwa wafanyabiashara wakubwa hasa baada ya kuzinduliwa
kwa sekta ya mafuta na gesi.
“Rwanda tayari imeanzisha kituo kama hicho, kimesaidia kutatua migogoro ya kibiashara dhidi ya wawekezaji na wafanyabiashara,” alisema.
Alisema hayo juzi, wakati akielezea
maandalizi ya mkutano wa kimataiafa wa usuhuhishi wa migogoro ya
kibiashara utakaofanyika jijini
Dar es Salaam, Aprili 9 - 10 mwaka huu.Simbeye alisema lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kutatua migogoro
ya kibiashara na kijamii nje ya
mahakama bila kufikishwa kwa kesi hizo mahakamani.
“Mkutano huu utashirikisha nchi za
Afrika Mashariki. Migogoro hiyo
itatatuliwa bila kesi kufikishwa
mahakamani kwa sababu tunaona
mashauri mengi yanatumia muda mrefu kutolewa hukumu lakini tukishiriana na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika
(TLS) na TPSF tunaweza kutatua
migogoro hiyo nje ya mahakama,”
alisema Simbeye.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Kaleb Gamaya alisema kupitia mkutano huo, washiriki watapata nafasi ya kuangalia jinsi ya kutatua migogoro nje ya utaratibu wa mahakama kama nchi zilizoendelea zinavyofanya.
“Usuluhishi wa migogoro unaofanyika mahakamani unaweza kumalizika baada ya miaka mitatu, hivyo kibiashara unakuwa umeathiri uchumi kwa sababu ya muda wa kupitia mashauri, ndiyo maana tukaona kuna haja ya kujitosa
kuanzisha utaratibu huu,” alisema
Gamaya.Aliongeza: “Lengo la TLS ni kujadili na kushawishi wanachama wetu kuwapo katika mkutano huu na washiriki watapata elimu na faida ya usuluhishi nje ya mahakama,” alisema.
Alisema mkutano huo wa tatu kufanyika Afrika, utajadili migogoro ya mafuta na gesi kwa sababu ni kitu kipya nchini na kwamba mikutano kama hiyo ilishawahi
kufanyika Nairobi na Addis Ababa
miaka mitatu iliyopita.
Mratibu wa mkutano huo kutoka
Mtandao wa kibiashara wa Afrika
Mashariki, Martha Yeronimo alisema watu zaidi ya 200 wanatarajia kushiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Toa maoni yako kupitia
Ochec54@gmail.com

Kwafursa na ushauri wa biashara piga simu +255 657 199 199

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments