BOKO HARAMU MAJI SHINGONI
Rais wa Nigeria,
Mohammadu Buhari, amesema kuwa majeshi yake yanakaribia kulishinda
kundi la kiislam , Boko Haram. Rais Buhari ameeleza kuwa kundi hilo
halina uwezo tena wa kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali
ama maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kwamba visa vya kujitoa
muhanga vimepungua .
Boko Haram wanaripotiwa kuendesha mashambulizi zaidi ya mia moja na kuua watu zaidi ya elfu moja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita .
Ikumbukwe kwamba ,wakati wa kampeni zake kuelekea uchaguzi nchini Nigeria,Rais Buhari alitoa ahadi ya kupambana na kundi la Boko Haram mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu.
Category:
0 comments