Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni ya reli Tanzania
(RAHCO) Benhadard Tito.
Mhandisi Tito amelazimishwa kukaa kando
ilikufanikisha uchunguzi katika utaratibu uliotumika wakati wa utoaji
wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
Rais Magufuli alichukua hatua hiyo kali baada ya mkutano na wadau wanaohusika na ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”
Uchunguzi wa kimsingi unaelekezwa kwa utoaji wa zabuni hiyo inayokisiwa kugharimu takriban dola milioni $14.
Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais
Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali. Sasa Magufuli al maarufu "The Bulldozer" ameiagiza
mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua
hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo
endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.
Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments