TANZANIA:RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AONGEZA MAKALI ZAIDI
Rais wa Tanzania John Magufuli
amevunja bodi simamizi ya bandari siku chache baada ya kupatikana kwa
makontena ambayo hayakuwa yamelipiwa ushuru bandari ya Dar es Salaam.
Tangazo la kuvunjwa kwa bodi hiyo limetolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kwenye kikao na wanahabari.
Kampuni 43 ziligunduliwa kuhusika katika makontena hayo.
Prof
Joseph Msambichaka ameondolewa kutoka kwa wadhifa wake kama mwenyekiti
wa bodi ya bandari sawa na Bw Awadhi Massawe ambaye amekuwa akihudumu
kama mkurugenzi mkuu.
Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dkt Shaban
Mwinjaka pia ameondolewa wadhifani "kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa
kazi nyingine".
Bw Kassim alifanya ziara ya kushtukiwa wiki
iliyopita katika bandari ya Dar es Salaam na ndipo akagundua makontena
329 yalipitishwa bila kulipiwa kodi kinyume na utaratibu wa bandarini.
Waziri
huyo mkuu anasema ripoti ya ukaguzi wa ndani iliyotolewa Julai 30 mwaka
huu ilionyesha makontena 2,387 yalipitishwa bandarini kinyume cha
utaratibu kati ya Machi na Septemba 2014.
"Serikali haitavumilia
kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo
au kuiibia serikali kwa namna yoyote kwa manufaa ya wachache,” amesema
Bw Majaliwa.
Miongoni mwa hatua alizochukua Bw Majaliwa ni kuagiza
kubadilishwa kwa mfumo wa malipo hadi mfumo wa kielektroniki ambao
unafaa kuwa umekamilika kufikia Ijumaa wiki hii.
Waziri mkuu huyo pia amewasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu.
Category:
0 comments