Home �
� KAMANDA WA IS ANUSURIKA KIFO KWENYE SHAMBULIZI LA WAMEREKANI
ZePLAN |
15:00:00 |
0
comments
Kundi moja la wachunguzi linasema
kuwa kamanda mmoja wa ngazi za juu wa kundi la Islamic State alijeruhiwa
vibaya lakini hakuuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa hivi
karibuni kaskazini mashariki mwa Syria.
Siku ya Jumanne,maafisa wa
ulinzi wa Marekani walisema kuwa Tarkhan Batiravshili,raia wa Georgia
anayejulikana kama Omar Shishani alifariki katika shambulio hilo karibu
na Shaddadi siku ya Ijumaa.
Lakini kundi la wachunguzi hao nchini
Syria lililo na makao yake makuu nchini Uingereza limesema kuwa lina
habari kwamba alichukuliwa na kupelekwa kupata matibabu mjini Raqqa.
Hakuna tamko lolote kutoka kwa IS kuhusu ripoti hiyo ya kifo cha Shishani.
Mwaka
uliopita ,Marekani ilitowa zawadi ya dola milioni 5 kwa yeyote yule
ambaye angetoa habari za Shishani ambaye inasema ameshikilia nyadhfa
kadhaa katika kundi hilo ikiwemo uwaziri wa vita.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
0 comments